Tuesday, 26 August 2014

Baada ya kurudi Shinyanga,Stand United yasema iko imara kwa ajili ya VPL.

Klabu ya Stand United ya mkoani Shinyanga iliyopanda ligi kuu soka Tanzania Bara (VPL) msimu huu imemaliza  ziara yake ya kukipima kikosi chake baada ya kufanya ziara mkoani Mwanza na Geita.

Akizungumza na Sports4lifetz msemaji wa Klabu hiyo Isack Edward  amesema kuwa klabu yao imefika mkoani Shinyanga jana (Agosti 25) baada ya kucheza michezo sita ikiwa kule kanda ya ziwa na ameongeza kuwa katika michezo hiyo wameshinda zote.

Lengo kuu la ziara hiyo ni kutangaza klabu kanda ya ziwa na pia kupata timu bora ya mashindano ya ligi kuu Mashindano ambayo yataanza kunguruma Septemba 20 na wao  kucheza na Ndanda FC.

Isack amesema kuwa Stendi United imepata kikosi imara baada ya kucheza michezo hiyo na kudai kuwa waalimu Masaja na Billal  wana imani klabu yao ina asilimia 60 ya ubora hadi sasa.

Ikiwa huko Mwanza klabu hiyo ikiwa na wachezaji pamoja na viongozi ilimtembelea aliyekuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars Silvester Marsh ambaye anasumbuliwa na maradhi Kwa kutambua umuhimu wake wa kujitolea kwa hali na Mali katika kuendeleza Soka la Tanzania.

Stand United imesema kuwa inatambua  mchango mkubwa wa Marsh ambaye alifanikisha timu kupanda daraja na kucheza ligi kuu ya Tanzania(VPL).


Ligi kuu soka Tanzania Bara itaanza  Septemba 20 mwaka huu ambapo Stand United watakaoikaribisha Ndanda ya Mtwara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

 Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC wataanza na Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Yanga SC  wataanza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro siku hiyo.

Mbeya City wataanza na JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Sokoine, Mbeya 
Simba SC wataanza na Coastal Union ya Tanga Septemba 21, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu zitakuwa kati ya  Mgambo JKT wataikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

0 comments:

Post a Comment