Tuesday, 26 August 2014

Maajabu,mshabiki wa Liverpool mkoani Tabora amnga'ata wa Manchester City.

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni,wakati mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza Ukiendelea jana mchezo kati ya Manchester City na Liverpool,mshabiki mmoja wa Manchester city mkoani Tabora ameng'atwa na mwenzake wa Liverpool.

Tukio hilo limetokea katika kata ya Goweko wilayani Uyui mkoani hapa ambapo Zola Gadaffi mshabiki wa klabu ya Liverpool nchini Tanzania alimng'ata mshabiki wa Manchester City bwana Ibrahim Haruna eneo la shavuni.

Taarifa zilizonaswa na Spors4lifetz hii leo ni kwamba Tukio hilo ambalo liliwashangaza mashabiki wengi katika ukumbi moja kule Uyui lilianza pale Ibrahim Haruna aliposhangilia bao la tatu lililofungwa na Sergio Aguero na kumchikiza Zola Gadafi ambaye aliruka moja kwa moja mpaka shavuni.

Wakati mashabiki wa Italia wakiwa na kumbukumbu ya aliyekuwa mchezaji wa Liverpool Luis Suarez kumng'ata meno Beki Chiellini wa Italia,sasa ni zamu ya mshabiki huyo wa Liverpol kugeuka kuwa Suarez.

Wadau waliokuwepo ukumbini pale waliamua ugomvi huo na leo asubuhi Ibrahim Haruna aliweza kufika hospitalini ili kupata matibabu.

Bwana Haruna amesema kuwa amemsamehe rafiki yake huyo Zola kwa kuwa yale ni mambo ya soka.

0 comments:

Post a Comment