Tuesday, 26 August 2014

Kikosi cha Taifa Stars chatajwa,kucheza na Morocco Septemba 5.

Kocha mkuu wa timu ya Tanzania,Taifa Stars Mart Nooij ametaja kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Morocco utakaochezwa Septemba 5, mwaka huu nchini Morocco.

Wachezaji walioitwa ni makipa; Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadini Ali (Azam).

Mabeki ni Said Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari Kapombe (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Joram Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).

Viungo; Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na Haruna Chanongo (Simba).

Washambuliaji; John Bocco (Azam), Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma Liuzio ZESCO, Zambia).

Kikosi hicho kinatarajiwa kuingia kambini Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) mchana katika hoteli ya Accomondia mjini Dar es Salaam na kitakuwa kikifanya mazoezi Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment