Boateng na Muntari nje kikosi cha Ghana kufuzu AFCON 2015.
Kevin Prince Boateng na Sulley Muntari, ambao walifukuzwa katika kambi ya timu ya taifa ya Ghana Kwa utovu wa nidhamu wakati wa kombe la dunia kule Brazil wameachwa katika kikosi cha Nchi hiyo kufuzu AFCON 2015.Taarifa zilizonaswa na Sports4lifetz kupitia mtandao wa FA ya Ghana ni kwamba Pia Michael Essien, ambaye alilalamika kuhusu kutocheza kule Brazil ameachwa sambamba na kiungo Albert Adomah na golkipa Adam Kwarasey.
Kocha wa Ghana Kwesi Appiah amemwita mchezaji wa klabu ya Leicester City Jeffery Schlupp na David Accam, anayecheza soka nchini Sweden, ambao hawakwepo katika kikosi cha kombe la dunia.
Blacks Stars itacheza na Uganda Septemba 5 mjini Kumasi na baadaye kusafiri hadi Togo Siku tano zijazo
KIKOSI KAMILI: Makipa: Stephen Adams (Aduana Stars), Razak Braimah (Mirandes), Fatau Dauda (Chippa United)
Walinzi: Harrison Afful (Esperance), Mohammed Awal (Maritzburg United), John Boye (Erciyesspor), Jonathan Mensah (Evian Thonon Gaillard FC), Daniel Opare (FC Porto), Baba Rahman (FC Augsburg), Jeffery Schlupp (Leicester City)
Viungo: Afriyie Acquah (Parma), Emmanuel Agyemang Badu (Udinese), Kwadwo Asamoah (Juventus), Christian Atsu (Everton), Andre Ayew (Olympique de Marseille), Yusif Chibsah (Sassuolo), Edwin Gyimah (Mpumalanga Black Aces), Rabiu Mohammed (Kuban Krasnodar), Asante Solomon (TP Mazembe Englebert), Mubarak Wakaso (Rubin Kazan)
Washambuliaji: David Accam (Helsingborg), Jordan Ayew (Lorient), Asamoah Gyan (Al Ain), Abdul Majeed Waris (Spartak Moscow).
0 comments:
Post a Comment