Thursday, 21 August 2014

Rojo asaini miaka minne Manchester United.

Mlinzi  raia wa Argentina Faustino Marcos Alberto Rojo amesaini Mkataba wa miaka minne ndani ya klabu ya Manchester United  baada ya kufuzu vipimo vya afya na kuafiki vipengele vya mkataba binafasi.
Mlinzi huyo aliyetokea  Sporting Lisbon, amenaswa kwa dau la Pauni Milioni 16.
Rojo atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na United msimu huu baada ya Ander Herrera na Luke Shaw,na atavaa jezi namba tano iliyokuwa inavaiwa na Rio Ferdinand.
Louis van Gaal ametoa kipaumbele kwa usajili wa beki huyo mtumia mguu wa kushoto, Rojo, mwenye umri wa miaka 24, kufuatia kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England Jumamois na Swansea.
Winga Luis Nani, aliyejiunga na United kutoka Sporting kwa Pauni Milioni 17 mwaka 2007, amerejeshwa kwa mkopo klabu yake hiyo ya zamani, ikiwa ni sehemu ya dili hilo la Rojo

0 comments:

Post a Comment