Thursday, 14 August 2014

Hatima ya Suarez kujulikana leo.

Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ya Michezo-CAS imedai kuwa hatima ya rufani ya mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Uruguay Luis Suarez kupinga adhabu aliyopewa kwa kumng’ata Giorgio Chiellini itajulikana leo (Alhamisi).
Suarez alifungiwa mechi tisa za kimataifa na kutojishughulisha na mambo yoyote yahusuyo soka kwa miezi minne baada ya kufanya tukio hilo katika mchezo wao wa hatua ya makundi dhidi ya  Italia  kwenye michuano ya Kombe la Dunia.
Baada ya kushindwa rufani yake kwa Shirikisho la Soka Duniani-FIF, mshambuliaji huyo wa Barcelona alipeleka kesi hiyo CAS ambayo ilisikiliza shauri hilo Ijumaa iliyopita.
Katika taarifa yake CAS jana  ilithibitisha kuwa itatoa uamuzi wake kuhusiana na rufani hiyo leo.

0 comments:

Post a Comment