Monday, 18 August 2014

John Cena anyang'anywa ubingwa mieleka,bingwa mpya huyu hapa,tazama picha zote.

Usiku wa kuamkia leo(Agosti 18) ulingo wa miereka ulishuhudia mipambano mbalimbali,ukiwemo mchezo baina ya John Cena na Brock Lesner.
Hatimaye John Cena amenyang'anywa ubingwa wa dunia wa mieleka baada ya kupigwa na Brock Lesner na kumaliza ule ubishi wa nani mkali kati ya wababe hao.
John Cena ambaye alikuwa anatetea ubingwa huo alikubali kushindwa lakini mwishoni madakatari waliingia ulingoni ili kumpatia huduma ya kwanza pale alipoumizwa na mbabe wake huyo yaani Brock Lesner.Tazama picha hizi.
Brock Lesner akiingia uwanjani na meneja wake Paul Heymen.

John Cena naye anaingia huku akionesha kitamba hicho kinachosihi kutokata tamaa.

Lesner alikuwa wa kwanza kumshambulia Cena

Cena anapigizwa chini

Cena akihesabiwa baada ya Lesner kuonekana kumzidi lakini Cena alichomoa.

Kwa mara nyingine tena Cena anashambuliwa

Zamu ya Brock kupewa kichapo

Lakini Brock alionekana imara zaidi,Cena ananyanyuliwa mzimamzima

Cena hala la kufanya.

Brock akimtazama kwa dharau Cena baada ya kumshindilia vipigo mfululizo

Cena anashindwa kuonesha makali,anawekwa begani kwa mara nyingine tena

Cena analipiza,Brock anaenda chini hapo.

Siri ya ushindi ni meneja huyu wa Brock,anaitwa Paul Heymen

Cena anajaribu kumkatalia Brock

Mwamuzi anahesabu kama Cena ataendelea na mchezo huo

Cena alizidiwa sana na mbabe huyu aliyempiga pia Undertaker mapema mwaka huu.

Cena anajaribu kukwepa mapigo hayo lakini bado Brock aliendelea kumnyanyasa

Cena aliamka na kuweza kumpiga hii staili Brock

Bingwa mpya ameshinda

Brock Lesner ametangazwa kuwa bingwa wa dunia baada ya kumpiga Cena.

Madakari wanamsaidia Cena baada ya kipigo hicho,Brock LESNER ndiye bingwa mpya kwa sasa 
.



0 comments:

Post a Comment