Kocha wa Barcelona Luis Enrique amesema kuwa mshambulizi wao mpya Luis Suarez ataruhusiwa kucheza leo.
Hiyo inafuatia baada ya kupigwa marufuku ya kushiriki
mashindano yeyote ya soka na shirikisho la soka duniani FIFA kwa
kumng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini katika mechi ya kombe la
dunia dhidi ya Uruguay.
Kocha Enrique anasema kuwa
mshambulizi huyo wa Barcelona Luiz Suarez sasa ataruhusiwa kushiriki
mechi ya kirafiki leo kati ya Barcelona na Club Leon ya
kutoka Mexico kufuatia masharti mapya yaliyowekwa na mahakama ya rufaa
katika michezo CAS.
Kocha huyo anasema kuwa mshambulizi huyo wa Uruguay anaruhusiwa
kujifua pamoja na timu yake mbali na kushiriki katika mechi za kirafiki.
''Suarez amekuwa akifanya bidii sana na kujifua
pekee yake kwa hivyo ninaamini kuwa itakuwa vyema akipata dakika chache
angalau mbele ya mashabiki wa nyumbani''
Kufuatia rufaa yake katika mahakama ya rufaa
katika michezo haijabainika kikamilifu aliruhusiwa kufanya nini lakini Suarez anasubiri kwa hamu na ghamu uamuzi kamili kutoka kwa mahakama
hiyo
Suarez anaendelea kutumikia marufuku ya mechi 9 za
kimataifa na huenda mechi yake ya kwanza ikawa tarehe 26 oktoba dhidi ya
wapinzani wao wakuu Real madrid.
Suarez anatarajiwa kujulishwa rasmi kwa mashabiki wa Barcelona leo katika uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp.
0 comments:
Post a Comment