Kikosi cha Cameroon chatangazwa,Nahodha Eto'o aachwa tena.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Cameroon Volker Finke ametangaza kikosi chake kwa ajili ya kufuzu AFCON 2015 michezo dhidi ya DR Congo hapo September 6 na Ivory Coast September 10 bila ya nahodha wake Samuel Eto’o.Wachezaji wengine waliotemwa ni Aurelien Chedjou, Benoit Assou-Ekotto, Jean II Makoun, Achille Webo na Charles Itandje wakati mchezaji wa Barcelona Alexandre Song anatumikia adhabu ya michezo mitatu baada ya kufanya makosa kombe la dunia 2014 kule nchini Brazil.
Finke amewaita wachezaji 25, ambao wataanza kuingia kambini September 1 mjini Yaounde.
Cameroon imepangwa kundi C sambamba na Ivory Coast, DR Congo na Sierra Leone.
KIKOSI KAMILI
Makipa: Guy-Rolland Ndy Assembe (Guingamp, France), Pierre-Sylvain Abogo (Tonnerre de Yaounde), Fabrice Ondoua (FC Barcelona, Spain). Walinzi : Cedric Djeugoue (Coton Sport), Nicolas Nkoulou (Marseille, France), Joel Matip (Schalke 04, Germany), Gaetan Bong (Olympiakos, Greece), Frank Bagnack (FC Barcelona, Spain), Jerome Guihota (Valenciennes, France), Ambroise Oyongo Bitolo (New York Red Bulls, USA)
Viungo : Eyong Enoh (Antalyaspor, Turkey), Stephane Mbia (FC Seville, Spain), Landry Nguemo (sans club), Raoul Loé (Osasuna, Spain), Edgar Salli (Monaco, France), Georges Mandjeck (Kayseri Erciyesspor, Turkey), Guy-Christian Zock (Cosmos Bafia), Marc Kibong Mbamba (Konyaspor, Turkey)
Washambuliaji: Eric-Maxim Choupo Moting (Schalke 04, Germany), Benjamin Moukandjo (Nancy, France), Vincent Aboubakar (Lorient, France), Jean-Marie Dongou (FC Barcelona, Spain), Léonard Kweuke (Caykur Rizespor, Turkey), Clinton Njie (Lyon, France), Franck Etoundi (FC Zurich, Switzerland)
0 comments:
Post a Comment