Saturday, 23 August 2014

Di Maria kutua Manchester United,Kuvaa jezi namba 7.

Klabu ya Manchester United inakaribia kumnasa winga wa Real Madrid Ángel Fabián Di María Hernández kwa uhamisho ambao utavunja rekodi ndani ya Old traford.
Mchezaji huyo mwenye miaka 26 ni mchezaji ambaye aliwindwa sana na klabu hiyo inayofundishwa na mholanzi Louis Van Gaal.
Mtandao wa skysports na goal.com umeeleza kuwa  Di Maria atasajiliwa kwa kiasi kati ya 60-70 million sawa na  Euros (£48-56m) .Taarifa zinadai kuwa Di Maria amekubali dili hiyo na mazungumzo yanaendelea na atakwenda Old traford wiki ijayo.

Mchezaji huyo wa zamani wa  Benfica ni wazi kuwa huduma yake imekwisha ndani ya Madrid baada ya kocha Carlo Ancelotti kusema kuwa Di Maria  amegoma kuongeza mkataba  Bernabeu.
Ujio wa  James Rodriguez na Toni Kroos ndani ya Madrid umehamasisha zaidi  Di Maria  kujiunga na Manchester United.
Di Maria  atavaa jezi namba 7 ndani ya Man U jezi ambazo zimevaliwa na nyota David Beckham, Eric Cantona, Cristiano Ronaldo, George Best na Bryan Robson.
Sports4lifetz inafuatilia taarifa hizi kwa undani zaidi.
Wasifu wake
Jina kamili Ángel Fabián Di María Hernández
Kuzaliwa 14 February 1988 (miaka26)
Sehemu alipozaliwa Rosario, Argentina


Nafasi uwanjani Winga / kiungo mshambuliaji
Vilabu
Kwa sasa
Real Madrid
Namba 22
Vijana
1995–2005 Rosario Central
wakubwa
Mwaka Team Amecheza mara  (mabao)
2005–2007 Rosario Central 35 (6)
2007–2010 Benfica 76 (7)
2010– Real Madrid 124 (22)
Timu ya taifa
2007 Argentina U20 13 (3)
2008 Argentina U23 6 (2)
2008– Argentina 52 (10)

0 comments:

Post a Comment