Kombe la Kagame APR na El Merreikh leo fainali.
Klabu za APR ya Rwanda na El Merreikh ya Sudan zitakutana Leo Jumapili(Agosti 24) kwenye Fainali ya Mashindano ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Kagame.Timu hizi zitakutana baada ya kufuzu kwa Mikwaju ya Penati baada kwenda Sare kwenye Mechi zao za Nusu Fainali hapo ijumaa.
APR walitoka suluhu 0-0 na wenzao wa Rwanda Polisi katika Dakika 120 za Mchezo na kufuzu kwa Penati 4-2 huku Kipa wao Olivier Kwizera akiokoa Penati mbili.
Nao El Merreikh walitoka Sare 2-2 na KCC FC ya Uganda na kushinda kwa Penati 3-0.
Fainali itachezwa kwenye Uwanja wa Amahoro huko Kigali, Rwanda.
0 comments:
Post a Comment