Sunday, 24 August 2014

Sfaxien na Setif wameingia mtoano,leo ni Mazembe na AS Vita.

Klabu ya CS Sfaxien imepanda katika nafasi ya kwanza katika kundi la B ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya ES Setif mchezo uliopigwa jumamosi usiku.
Mchezo huo kwa ujumla ulikosa ufundi baada ya timu zote kucheza ovyo. Mchezaji  Ze Ondo alifungwa bao kwa upande wa ES Setif dakika ya  64.
Mchezaji Maaloul alisawazisha bao kwa upande wa Sfaxien.
Kwa matokea haya CS Sfaxien pamoja na ES Setif  watasonga hatua ya mtoano.
Leo jumapili Klabu ya TP Mazembe watavaana na mahasimu wao Vita ambao wameshangaza wengi baada ya kupenya katika kundi lililokuwa na timu kongwe kama Zamalek ya Misri na Al Ahly ya Sudan wakati Esperance (Tunisia) watapambana na Al Ahly Benghazi (Libya).



KUNDI  A









Pts
1TP Mazembe (Congo DR)






10
2AS Vita (Congo DR)






10
3Al Hilal (Sudan)






7
4Zamalek (Egypt)






4

KUNDI  B










Pts
1CS Sfaxien (Tunisia)






11
2ES Setif (Algeria)






10
3Esperance (Tunisia)






4
4Al Ahly Benghazi (Libya)






4

0 comments:

Post a Comment