Monday, 18 August 2014

Manchester United yakubali kumsainisha Rojo.

Klabu ya Manchester United imekubali dili la   €20 million kwa ajili ya kumnasa mlinzi wa Sporting  Marcos Rojo, huku mchezaji Nani akitolewa kwa mkopo.

Rojo atakwenda Old Trafford baada ya makubaliano ya muda mrefu baina ya vilabu hivyo , huku mchezaji huyo akiwaomba radhi wachezaji wenzake na mashabiki baada ya kugoma kufanya mazoezi wiki hii.
Inaonekana dili hilo litamfaidisha rais wa  Sporting bwana Bruno de Carvalho.

Rais huyo aligoma  kiasi cha  €20m kama kianzio kwa ajili ya  Rojo huku kampuni ya Doyen Sports, ambayo inamiliki asilimia 75 ya mchezaji huyo ikigoma pia.

Klabu ya  Sporting inahitaji kiasi cha  20%  kwenye  €5m kwa ajili ya  Rojo na kulipa klabu yake ya zamani ya  Spartak Moscow, na  75% itakwenda kwa Doyen, huku mchezaji huyo aliyecheza mchezo wa fainali kombe la dunia atauzwa kwa kiasi cha €20m.

0 comments:

Post a Comment