Tuesday, 19 August 2014

Robo fainali Kagame kuanza leo,Azam dimbani kesho.

Hatua ya Robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati, Kombe la Kagame, inaanza kutimua vumbi leo jumanne mjini Kigali, Rwanda.
Robo fainali ya kwanza itaanza majira ya 9:00 alasiri kwa kuwakutanisha wanyarwanda wawili, Polisi na Atletico.
Robo fainali ya pili itaanza majira ya saa 11:00 jioni ambapo timu mbili pinzani nchini Rwanda, Rayon Sport na APR zitachuana vikali.
Baada ya kuwafahamu washindi watakaocheza nusu fainali leo, robo fainali nyingine mbili zitapigwa kesho jumatano.
Jumanne
Police (Rwanda) v Atletico Olympique (Burundi)
Rayon Sport ([Rw) v APR (Rw)
Jumatano
Azam (Tanzania) v El Merreikh (Sudan)
KCCA (Uganda) v Atlabara (S.Sudan)
Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam fc watashuka dimbani kukabiliana na El Merreikh ya Sudan
Mechi nyingine ya kesho jumatano itawakutanisha KCC ya Uganda dhidi ya Altabara ya Sudan Kusini.

0 comments:

Post a Comment