Thursday, 14 August 2014

Ronaldo,Neuer na Robben kuwania mchezaji bora Ulaya 2014.

Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo,golkipa wa timu ya taifa ya Ujerumani Manuel Neuer pamoja na mholanzi  Arjen Robben ni wachezaji watatu waliotangazwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya.
Bodi ya Uefa imekutana leo(Alhamisi)na kutangaza majina ya wachezaji hao.
Neuer ametangazwa ikiwa ni mara baada ya jumapili hii kutangazwa kuwa mchezaji bora wa Ujerumani baada ya kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa dunia..
Kwa upande wa mreno Ronaldo alishindwa kuonesha makeke kule Brazil lakini aliisaidia Real Madrid kubeba ubingwa wa ulaya kwa vilabu yaani UEFA huku akiweka rekodi ya kufunga mabao 17. Real pia ilishinda ubingwa wa kombe la Hispania mwaka 2013-14 Robben alisaidia Uholanzi kumaliza katika nafasi ya tatu kule Brazil na kubeba mataji mawili akiwa na mabingwa wa  Bundesliga ,Munich.
Mshindi atatangazwa siku ya  August 28 siku hiyo pia makundi ya ligi ya mabingwa ulaya yatatangazwa.

0 comments:

Post a Comment