Thursday, 14 August 2014

Basi la TFF lakamatwa na madalali.

Basi la Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekamatwa na madalali kwa amri ya mahakama kutokana na deni la sh milioni 140 ambalo shirikisho la soka nchini linadaiwa hadi litakapolipwa,imeleza taarifa ya mtandao wa Binzubeiry.
Amri hiyo imetokana na deni hilo la kampuni ya Punchline ya Kenya iliyokuwa ikichapa tiketi za kuingilia uwanjani kuanzia mwaka 2007. Hadi sasa tff imeshalipa sh. milioni 70 katika deni hilo.
Tff imesema inafanya jitihada  ili kumaliza deni hilo. Pia kuchunguza mwenendo mzima uliosababisha kuwepo deni hilo.

0 comments:

Post a Comment