Wajerumani wa Arsenal watua mazoezini.
Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Olivier Giroud amesema kuwa Arsenal itafanya vizuri katika msimu huu baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa ngao ya jamii.Wachezaji wa Ujerumani ambao wamenyakua ubingwa wa dunia na timu yao ya taifa Lukas Podolski, Per Mertesacker na Mesut Ozil mawerudi rasmi mazoezini tayari kwa mchezo wa ufunguzi wa ligi ya Uingereza dhidi ya Crystal Palace.
Giroud amesema kuwa iwapo wajerumani hao wakiongeza nguvu klabuni timu itafanya vizuri hadi msimu umalizike hapo mwezi Mei.
Giroud alifunga bao la tatu wakati Arsenal ikibeba ubingwa wa ngao ya jamii
0 comments:
Post a Comment