Ghana kumteua mtoa ushauri benchi la timu ya taifa.
Shirikisho la soka nchini Ghana (GFA) imeunda kamati ya watu watatu ili kumchagua mtoa ushauri wa benchi la timu ya taifa ya nchi hiyo, Black Stars.
Maamuzi hayo yamefanyika jana wakati kamati ya utendaji ilipokutana kwa ajili ya timu ya taifa.Makamu wa rais wa GFA Fred Crentsil ataongoza kamati hiyo sambamba na Fred Pappoe pamoja na Francis Oti Akenteng.
Kocha wa Black Stars Kwesi Appiah naye pia atahusika katika kutoa ushauri kwa kamati hiyo.
Kamati hiyo itatoa majibu kwenda kamati ya utendaji wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment