Monday, 29 September 2014

Baada ya kutimuliwa Esperance,Krol kocha mpya Al-Ahli.

Mchezaji na nahodha  wa zamani wa Uholanzi Ruud Krol ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Al-Ahli Tripoli
Kocha huyo ameteuliwa ikiwa ni miezi minne tu tokea achukue hatamu ya kuifundisha klabu ya  Esperance, ya Tunisia na alitimuliwa baada ya klabu kufanya vibaya michuano ya Klabu bingwa Afrika.

Krol ana uzoefu na soka la bara la Africa baada ya kufundisha soka akiwa Misri,Afrika kusini na Tunisia.
 
Atajiunga na mabingwa hao mara 11 wa Libya  Novemba 1.

Baada ya kupata nafasi hiyo Krol amesema kuwa anajua sana soka la Afrika kwa hiyo kwenda kufundisha soka Libya hakumpi taabu yoyote.

Nyota huyo wa zamani,65 alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Tunisia ambapo timu iligaragazwa na Cameroon  4-1  kufuzu kombe la dunia 2014 Brazil.

Krol amesema kuwa hali ya machafuko ya kisiasa nchini Libya si tatizo kwake.

0 comments:

Post a Comment