Monday, 29 September 2014

Hazard asema hana mpango wa kwenda PSG.

Mchezaji wa klabu ya Chelsea Eden Hazard amekanusha taarifa za kuondoka Chelsea kwenda kujiunga na matajiri wa Ufaransa Paris Saint-Germain – licha ya kuvutiwa na matajiri hao.
 
Nyota huyo aliyeshinda tuzo ya mchezaji kijana ya PFA msimu uliopita kwa muda mrefu alihusishwa kujiunga na kikosi cha  Laurent Blanc majira ya kiangazi mwaka huu, lakini Jose Mourinho alisema atasikiliza ofa itayozidi paundi milioni 150 ili kumuachia mchezaji wake.
 
Licha ya kuanzia soka lake Ligue 1 kabla ya kujiunga na Chelsea kwa paundi milioni 32 mwaka 2012, Hazard alisema hana nia ya kuondoka klabuni hapo kurudi alikotoka.
 
Kutokana na kiwango chake, The Blues  wanatarajia kumzawadia namba 10 huyo mkataba wa miaka mitano ambapo atalipwa mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki na anatarajia kutia saini mwezi ujao.

Mapema wiki hii klabu ya Chelsea  ilitangaza kuwa ina nia ya kumwachia Ramires kwenda kujiunga na Real Madrid ili imnase mchezaji wa Everton,Ross Barkley.
 
Chelsea inahitaji kiasi cha  £25 million kwa ajili ya Mbrazil huyo na imeandaa  kiasi cha  £30 million kwa ajili ya  Barkley,ambaye mwenyewe amekiri kuitamani Chelsea kuliko  Manchester.

0 comments:

Post a Comment