Tuesday, 30 September 2014

UEFA kuendelea leo,Drogba hatacheza kisa kuwasubiri Arsenal.

Ligi ya mabingwa barani Ulaya,UEFA hatua ya makundi  inaendelea leo katika viwanja mbalimbali.

Kuelekea michezo hiyo klabu ya Chelsea imeamua kumbakisha nyota Didier Drogba jijini London wakati klabu hiyo ikisafiri hadi Lisbon, Ureno  kucheza na Sporting Lisbon.

Chelsea haikutamka lolote kwanini ameachwa hasa ukizingatia hali ya  Diego Costa ambaye anakabiliwa na matatizo ya Msuli wa Pajani kiasi cha kushindwa kufanya Mazoezi kama ilivyoelezwa na Jose Mourinho.

Lakini wadadisi wanadai kuwa Drogba ameachwa ili ajifue vema kwa ajili ya mchezo wa wikiendi hii kati ya Chelsea na Arsenal huku ikidaiwa kuwa Drogba ana rekodi nzuri ya kuwafunga Arsenal.

Mabingwa wa soka nchini Uingereza Manchester City ambao watakuwa wenyeji wa AS Roma ya Italia katika mchezo wa kundi E utakaofanyika katika Uwanja wa Etihad. 

City wataingia katika mchezo wakihitaji ushindi baada ya kupoteza mchezo wao kwanza waliochezwa na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich ambao walifungwa bao 1-0 huko Allianz Arena.

RATIBA SEPTEMBA 30
CSKA MoscowvFC Bayern MünchenArena Khimki19:00
FC Schalke 04vNK MariborVELTINS-Arena21:45

Paris Saint GermainvBarcelonaParc des Princes21:45

Shakhtar DonetskvFC PortoArena Lviv21:45

Sporting LisbonvChelseaEstadio José Alvalade21:45

BATE BorisovvAthletic ClubBorisov Arena21:45

Manchester CityvRomaEtihad Stadium21:45

APOEL NicosiavAjaxGSP Stadium21:45


0 comments:

Post a Comment