Baada ya sare ya 1-1 Pelegrini asema Chelsea ilicheza kama timu ndogo.
Kocha wa klabu ya Manchester City Manuel Pellegrini amesema Chelsea walicheza kama timu ndogo wakati wa Mechi yao ya Jumapili iliyochezwa Etihad na kutoka Sare 1-1 katika Ligi Kuu Uingereza.Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard, alisawazishia Man City baada ya Chelsea kuongoza kupitia bao la Andre Schurrle.
Akiongea baada ya Mechi hiyo, Pellegrin, mwenye Miaka 61, alisema: “Nadhani tulicheza Dakika 90 na Timu ndogo iliyokuwa ikijihami. Siwezi kuwa na furaha kucheza namna ile. Wachezaji 10 walijihami upande wao wa Uwanja na walifunga Goli kwa kushtukiza na wakaendelea kujihami hadi mwisho! ”
Pellegrini aliifananisha Chelsea na Stoke City ambayo Mwezi uliopita iliifunga City 1-0 Uwanjani Etihad.
Mpambano huo ulimalizika kwa Man city kubaki na wachezaji 10 baada ya Zabaleta kupewa kadi nyekundu.
0 comments:
Post a Comment