Klabu ya JS Kabylie lupango ya soka miaka miwili,ni baada ya Ebosse kuuawa.
Klabu ya JS Kabylie inayocheza ligi kuu ya nchini Algeria imefungiwa kutojihusisha na shughjuli za soka kwa miaka miwili baada ya kutokea mauaji ya mchezaji raia wa Camerooni, Albert Ebosse.Taarifa zilizonaswa na Sports4lifeTz zinadai kuwa uamuzi huo ulitolewa baada ya kamati ya utendaji ya CAF kukutana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Kabylie ilimaliza nafasi ya pili msimu uliomalizika katika ligi ya Algeria na na ingeshiriki mashindano ya CAF 2015.
Ebosse alifariki hospitalini mwezi uliopita baada ya kupigwa na kitu kilichorushwa kutoka jukwaani wakati wa mechi ya Ligi ya Algeria, timu yake JS Kabylie ikipambana na USM Alger.
Marehemu Ebosse ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 24 aliwahishwa hospitalini lakini akaaga dunia.
Ebosse aliifungia bao Kabylie katika mechi hiyo iliyoisha kwa kipigo cha nyumbani cha 2-1 kutoka kwa USM Alger.
Klabu ya Kabylie inapatikana upande wa kaskazini mwa mji wa Tizi Ouzou imebeba mara mbili ubingwa wa Algeria kombe moja la shirikisho barani Afrika na kombe la CAF mara tatu.
0 comments:
Post a Comment