Franck Ribery lazima aadhibiwe,kwanini amestaafu soka?-Platini.
Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini haelewi kwanini mchezaji wa Ufaransa Franck Ribery amechukua uamuzi wa kustaafu soka la kimataifa na kudai kuwa lazima aadhibiwe kama hataki kucheza.Winga huyo wa Bayern Munich alijitoa katika kikosi cha Ufaransa kabla ya kwenda kucheza kombe la dunia na baada ya michuano kumalizika alitangaza kustaafu rasmi soka la kimataifa.
Platini ameshangazwa sana na uamuzi huo na kudai kuwa iwapo akiitwa tena na kocha Didier Deschamps na asipojiunga na timu lazima apewe adhabu kubwa.
Mchezaji mwenzake wa Munich Philip Lahm alitangaza kujiuzulu kucheza soka la kimataifa na Platini akaelezea hilo na kusema ni makubaliano baina ya kocha Low na Lahm.
Amesema kuwa haelewi chochote mpaka sasa kwanini Ribery achukue uamuzi huo.
Platini amesema iwapo Ribery hatarudi timu ya taifa atafungiwa michezo mitatu ya Bayern Munich na kusema kuwa kamwe hataelewa utetezi wa mchezaji huyo .
Mshikemshike wa Michuano mikubwa barani Ulaya kwa mwaka 2016 yaani EURO 2016 utachukua nafasi nchini Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment