Sunday, 7 September 2014

Mjapan amtupa nje Djockovic na kutinga fainali ya US Open.

Mcheza tennis Kei Nishikori ameharibu mipango ya mcheza tennis namba 1 duniani  Novak Djokovic baada ya kumshinda katika michezo ya wazi ya Marekani maarufu kama (US Open)  na kuwa mjapan wa kwanza  kucheza hatua ya fainali.

Mchezo huo uliomalizika muda mfupi uliopita ulishuhudiwa Nishikori akishinda kwa ushindi wa  6-4 1-6 7-6 (7-4) 6-3.
Mcheza tennis huyo mwenye miaka 24 atacheza na  Roger Federer au Marin Cilic katika fainali siku ya kesho (Jumatatu).

Nishikori anayeshikilia nafasi ya 10, anafundishwa na  Michael Chang.
Baada ya mchezo huo kumalizika alisema kuwa ni furaha sana kumshinda mchezaji namba moja duniani.

0 comments:

Post a Comment