Wednesday, 17 September 2014

Gutierrez anaenda kupatiwa matibabu ya Kansa.

Kiungo wa klabu ya Newcastle United Jonas Gutierrez hii leo amewashukuru mashabiki wake kwa sapoti waliyompa baada ya kutua nchini  Argentina kwa ajili ya matibabu ya kansa ya korodani.

"Nashukuruni sana kwa ujumbe wenu.Kwa sasa naangalia mbali zaidi," alisema mchezaji huyo mwenye miaka 31 katika ukurasa wake wa  Twitter 

Gutierrez amegundulika kuwa ana maradhi hayo na kusema kuwa alipopata majibu alilia sana.
"Nimefika hapa kwa gharama zangu , japo nina mkataba na  Newcastle.
"Fedha sio muhimu. Kitu muhimu ni afya yangu." alisema Gutierrez.

Gutierrez alijiunga na  Newcastle akitokea klabu ya  Real Mallorca ya Hispania mwaka 2008. Amecheza michezo 177 na kufunga mabao 10 .

Gutierrez kwa sasa anachezea Norwich City kwa mkopo na hakucheza tokea mwaka  2014-15.

0 comments:

Post a Comment