Dunga ataja kikosi cha kuivaa Argentina,Maicon na Marcelo nje.
Kocha wa Brazil Dunga ametaja kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya mechi za kirafiki dhidi ya Argentina na Japan mwezi ujao.Mabingwa hao mara tano wa kombe la dunia watakwenda mjini Beijing hapo Octoba 11 kupambana na makamu bingwa wa kombe la dunia na kuelekea Singapore kupepetana na Japan Octoba 14.
Kuna wachezaji wawili tu walioitwa kwenye kikosi hiki tofauti na ile ya awali ambapo mchezaji wa Inter Dodo na mchezaji wa CSKA Mario Fernandes wameitwa kuziba nafasi za Marcelo na Maicon
KIKOSI KAMILI
Makipa: Jefferson (Botafogo), Rafael Cabral (Napoli).
Walinzi: David Luiz (Paris Saint-Germain), Marquinhos (Paris Saint-Germain), Gil (Corinthians), Miranda (Atletico Madrid), Dodo (Internacional), Filipe Luis (Chelsea), Mario Fernandes (CSKA), Danilo (FC Porto).
Viungo: Luiz Gustavo (Wolfsburg), Elias (Corinthians), Fernandinho (Manchester City), Ramires (Chelsea), Willian (Chelsea), Everton Ribeiro (Cruzeiro), Oscar (Chelsea), Coutinho (Liverpool).
Washambuliaji: Ricardo Goulart (Cruzeiro), Robinho (Santos), Neymar (Barcelona), Diego Tardelli (Atletico MG).
0 comments:
Post a Comment