Monday, 29 September 2014

Rooney aomba msamaha,Sakho kuchunguzwa baada ya kumpiga kichwa Shaw.

Nahodha wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney amewaomba radhi Wachezaji wenzake kwa kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya Ligi Kuu Uingereza  Jumamosi huko Old Trafford wakati Manchester United ikishinda 2-1 dhidi ya  West Ham.

Rooney alipewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 54 na mwamuzi  Lee Mason kwa kumchezea Rafu Stewart Downing na amesema hana mpango wa kukata Rufaa.

Kutokana na Kadi hiyo, Rooney atazikosa Mechi 3 za Ligi ambazo ni dhidi ya Everton, WBA na Chelsea na atarejea Uwanjani Novemba 2 kwenye Dabi ya Jiji la Manchester dhidi ya Man City kwenye Mechi ya Ligi Kuu Uingereza.

Kwa upande wa kocha wa  Man United, Louis van Gaal, alikiri kuwa ilistahili kwani alikosea jinsi ya kumsimamisha Downing aliekuwa akichanja mbuga .

Mwenyewe Rooney ameeleza: “Nilimwona Mchezaji wa West Ham akifanya kaunta ataki na mimi nilijaribu kuvunja hiyo lakini nilikosea namna ya kumzuia. Nimefarijika wenzangu walilinda Bao zetu na tumeshinda.”

Hata hivyo Mechi hiyo pia imekumbwa na tukio jingine la utata kwani Straika wa West Ham Diafra Sakho sasa anaweza kuadhibiwa na FA baada ya kudaiwa kumpiga Kichwa Beki wa Man United Luke Shaw wakati hawakuwa na Mpira na tukio hilo kutoonwa na mwamuzi Lee Mason.

0 comments:

Post a Comment