Kozi Ukocha leseni A kufungwa leo na mbunge Ntanda.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mheshimiwa Said Mtanda anatarajia kufunga kozi ya ukocha ya Leseni A ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) inayomalizika leo (Septemba 7 mwaka huu).Hafla hiyo ya ufungaji wa kozi hiyo iliyoshirikisha makocha 22 itafanyika saa 7 mchana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam.
Kozi hiyo ya siku tano iliyokuwa chini ya wakunzi wa CAF, Moatasim Mohamed Nasr kutoka Sudan na Sunday Kayuni wa Tanzania.
Wakati huohuo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wameandaa kozi ya ukufunzi wa utawala itakayofanyika Desemba mwaka huu.
Kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi kutoka FIFA itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Desemba 1 hadi 5 mwaka huu, ambapo sifa ya chini ya elimu kwa wanaotaka kushiriki ni kidato cha nne.
Kwa wanaotaka kushiriki kozi hiyo wanatakiwa kutuma maombi yao kwa Katibu Mkuu wa TFF. Mwisho wa kupokea maombi hayo ni Septemba 12 mwaka huu ambapo wanatakiwa pia kuwasilisha nakala za vyeti vyao vya kitaaluma.
0 comments:
Post a Comment