Simba yaipiga 3-0 Gor Mahia,Kiongera awaliza ndugu zake.
Wekundu wa Msimbazi Simba wamefanikiwa kuwatungua mabao 3-0 mabingwa wa ligi kuu nchini Kenya (KPL), Gor Mahia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa jana katika Taifa jijini Dar es salaam.Bao la kwanza la Simba lilifungwa katika dakika ya 55 kipindi cha pili na mshambuliaji mpya kutoka Kenya, Paul Kiongera baada ya kumalizia pasi murua iliyochongwa na Mganda, Emmanuel Anord Okwi.
Okwi katika dakika ya 73 alipiga shuti kali lililotemwa na kipa wa Gor Mahia, Patrick Odhiambo na mpira kumkuta Ramadhan Singano ‘Messi’ aliyefanya kweli na kuzamisha mpira nyavuni na kuandika bao la pili.
Simba waliendelea kuonesha kiwango kizuri na kulisaka lango la Gor Mahia na katika dakika ya 77 waliandika bao la tatu kupitia kwa Paul Kiongera.
Baada ya kufungwa kwa bao la tatu baadhi ya mashabiki wanaokalia jukwaa la kusini mwa uwanja wa Taifa na waliokuwa wanaishangalia Gor Mahia walianza kuondoka uwanjani.
0 comments:
Post a Comment