Monday, 8 September 2014

Kufuzu EURO 2016 Mambo yameanza,Gibraltar yabamizwa 7.

Michezo ya kufuzu EURO 2016 imeanza jana ambapo mabingwa wa dunia Ujerumani wakicheza Mechi yao ya kwanza ya Mashindano rasmi tangu wachukue Kombe la Dunia hapo Julai 13 kwa kuichapa Argentina Bao 1-0, Jana Usiku walishinda 2-1 dhidi ya Scotland

Mabao ya Ujerumani yalifungwa Dakika ya 18 na Thomas Muller na Ikechi Anya kuisawazishia Scotland Dakika ya 66 baada ya kazi njema ya Nahodha Darren Fletcher.

Lakini Dakika 4 baadae Thomas Muller akawapa Ujerumani Bao la Pili baada kuunasa Mpira wa Kona.
MATOKEO:

Jumapili Septemba 7

Denmark 2 Armenia 1

Hungary 1 Northern Ireland 2

Georgia 1 Ireland 2

Germany 2 Scotland

Faroe Islands 1 Finland 3

Greece 0 Romania 1

Portugal 0 Albania 1

Gibraltar 0 Poland 7


Jumatatu Septemba 8
Mechi zote kupigwa saa 3(tatu) dk 45 usiku
 Russia v Liechtenstein

 Luxembourg v Belarus

Austria v Sweden

 San Marino v Lithuania

Spain v Macedonia

 Estonia v Slovenia

 Switzerland v England

 Ukraine v Slovakia
Montenegro v Moldova

0 comments:

Post a Comment