Serena William ni noma,abeba ubingwa wa 18
Mcheza tennis Serena Williams wa Marekani ametwaa ubingwa wa michuano ya wazi ya Marekani yaani US Open.Williams ameshinda katika mchezo uliofanyika usiku wa kuamkia leo baada ya kumtwanga Caroline Wozniacki wa Denmark kwa ushindi wa moja kwa moja.
Mpambano huo wa fainali ulipigwa mjini New York ambapo Serena ameshinda kwa seti 6-3, 6-3 na kujinyakulia ubingwa huo kwa mara ya 6.
Kwa sasa Serena ndiye mchezaji nambari 1 duniani kwa mchezo huo na pia bingwa mara 18 wa Grand Slam, amekuwa bingwa wa kombe hilo mara tatu mfululizo tangu mwaka 2012.
Baada ya mchezo kumalizikia,Wozniacki ambaye ni rafiki wa karibu wa Serena alimpongeza rafiki yake huyo baada ya mchezo na kusema alistahili ushindi huo kutokana na jinsi alivyocheza.
Mataji 18 ya Grand Slam za Serena Williams |
---|
Australian Open (5): 2003, 2005, 2007, 2009 and 2010 |
French Open (2): 2002 na 2013 |
Wimbledon (5): 2002, 2003, 2009, 2010 na 2012 |
US Open (6): 1999, 2002, 2008, 2012, 2013 na 2014 |
0 comments:
Post a Comment