Thursday, 25 September 2014

Liverpool wawekwa kikaangoni na UEFA.

Klabu  ya Liverpool inachunguzwa na UEFA kwa kudaiwa kuvunja sheria ya matumizi ya fedha.

Tangazo lililotolewa leo asubuhi imeeleza kuwa UEFA inapitia nyaraka mbalimbali ili kujua matumizi ya klabu hiyo.

Liverpool, Monaco, Inter Milan na Roma — ambao hawakuwepo katika michuano ya Ulaya msimu uliopita wametuma akaunti zao UEFA na sasa wanasubiri kuulizwa juu ya taarifa nyingine za kifedha.

Liverpool imepoteza kiasi cha  £50m kwa msimu wa mwaka   2012-13 na ilipata hasara ya kiasi cha   £40m kwa miezi 10 iliyopita.

Hakuna vikwazo watakavyowekewa kwa hatua hii, ingawa kifungo cha kutopata fedha za ligi ya mabingwa kinaweza kufuata.

0 comments:

Post a Comment