Chelsea iko tayari kumuuza Ramires kwenda Madrid
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali nchini Uingereza, klabu ya Chelsea iko tayari kumuuza mchezaji Ramires, ambaye anawindwa na mabingwa wa Ulaya klabu ya Real Madrid huku ikiwa na lengo la kumnunua Ross Barkley kutoka Everton.Madrid inayofundishwa na Carlo Ancelotti iko tayari kumnunua Ramires.
Chelsea maarufu kama the Blues inaweza ikafanikiwa kumnasa mchezaji huyo ambaye anawindwa na Manchester City lakini City itabanwa na sheria ya matumizi ya fedha.
Ramires ameanza michezo miwili tu ndani ya utawala wa Mourinho.
Chelsea inahitaji kiasi cha £25 million kwa ajili ya Mbrazil huyo na imeandaa kiasi cha £30 million kwa ajili ya Barkley,ambaye mwenyewe amekiri kuitamani Chelsea kuliko Manchester.
0 comments:
Post a Comment