Rekodi ya usajili Uingereza,Van Gaal aweka rekodi huku EPL ikitumia £835m,ni rekodi mpya.
Kwenye Siku ya mwisho, Falcao amehamia Man United kutoka AS Monaco kwa Mkopo kwa Pauni Milioni 6, Daley Blind kutoka Ajax na kutua Man United kwa Pauni Milioni 13.8 na Danny Welbeck kuuzwa na Man United kwa Arsenal kwa Pauni Milioni 16,imewafanya United washikilie rekodi ya usajili msimu huu.
Lakini mapema wiki hii United iliweka rekodi ya usajili mkubwa nchini Uingereza kwa kumnunua Angel Di Maria kwa kiasi cha £59.7m.
Wachambuzi wa uchumi wamedai kuwa kocha Louis van Gaal ametumia kiasi cha £150m na kuwa kocha wa kwanza msimu huu kutumia pesa nyingi katika usajili.
Liverpool imetumia kiasi cha euro mil 117 na Man city imetumia kiasi cha euro millioni 91.1,angalia jedwali hapo chini.
UHAMISHO WA FEDHA NYINGI KATIKA MSIMU HUU. |
---|
Angel Di Maria [Real Madrid - Manchester United] £59.7m |
Alexis Sanchez [Barcelona - Arsenal] £35m |
Diego Costa [Atletico Madrid - Chelsea] £32m |
Eliaquim Mangala [FC Porto - Manchester City] £32m |
Cesc Fabregas [Barcelona - Chelsea] £30m |
Ander Herrera [Athletic Bilbao - Manchester United] £29m |
Romelu Lukaku [Chelsea - Everton] £28m |
Luke Shaw [Southampton - Manchester United] £27m (Could rise to £31m) |
Adam Lallana [Southampton - Liverpool] £25m |
Dejan Lovren [Southampton - Liverpool] £20m |
Lazar Markovic [Benfica - Liverpool] £20m |
0 comments:
Post a Comment