"Ronaldo anarudi Manchester United,amechoshwa na Madrid"
Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon amedai Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo amechoshwa na Klabu yake hiyo na yupo mbioni kurejea Klabu yake ya zamani Manchester United.Ronaldo alisajiliwa kutoka Man United kwenda Real Madrid Mwaka 2008 wakati huo rais akiwa ni Ramon Calderon kwa Dau la Rekodi ya Dunia.
Na hivi sasa Calderon amedai uhusiano wa Ronaldo na Rais wa sasa wa Real, Florentino Pérez, umekuwa si mzuri hasa baada ya Klabu hiyo kuwauza Wachezaji wao Xabi Alonso kwa Bayern Munich na Angel di Maria kwa Man United.
Akiongea kwenye Kipindi cha TV, Alan Brazil Sports Breakfast, Calderon alisema: amesema kuwa Ronaldo amechoshwa na msimamo wa Rais wa sasa.
Rais huyo wa zamani alidai kuwa Ronaldo alipokuja Real alitegemea atakaa pamoja na Arjen Robben lakini Mchezaji huyo akauzwa.
Aliongeza: “Miaka miwili iliyopita Gonzalo Higuain akauzwa na hakupendezwa. Mwaka Jana alisema ni makosa kumuuza Mesut Ozil lakini nae akauzwa. Kitu cha mwisho kilichomkera sana sana ni kuuzwa kwa Xabi Alonso na Angel di Maria hivi karibuni.”
Huku kukiwa na ripoti kuwa Man United imeshaandaa mpango wa kumchukua tena Ronaldo, Calderon amedokeza hatashangazwa na hilo na kueleza: “Nilipomsaini Mwaka 2008 nakumbuka alisema ninaishukuru sana Manchester United. Alikuwa na wakati mzuri kule na alipenda kila kitu. Ni Klabu kubwa na bora.”
0 comments:
Post a Comment