Sir Alex Ferguson akutana na makocha UEFA ili kuwapa mafunzo.
Jana kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson alikutana na makocha mbalimbali wa Klabu kubwa Barani Ulaya katika Kikao cha makocha kilichofanyika Jumatano na Alhamisi kwenye Makao Makuu ya UEFA huko Nyon, Switzerland.Ferguson ndiye alikuwa Mwenyekiti na alikutana na makocha wawakiwemo Jose Mourinho, Manuel Pellegrini na Arsene Wenger lakini kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal hakuwepo.
Kwa sasa Ferguson ni Balozi wa UEFA na hilo limemfanya ahudhurie Kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Rais wa UEFA Michel Platini.
Louis van Gaal hakuwepo kwa vile wanaohudhuria ni wale tu ambao Timu zao zipo kwenye Mashindano ya UEFA.
Mkocha wengine wengine waliohudhuria ni Andre Villas-Boas, Rafael Bentiez na Carlo Ancelotti huku Meneja wa sasa Barcelona Luis Enrique alinaswa kuketi pamoja na kocha wa zamani wa Klabu hiyo Pep Guardiola ambaye sasa yupo Bayern Munich.
Kikao cha kwanza cha aina hii kufanyika ilikuwa ni Mwaka 1999 na safari hii miongoni mwa Wazungumzaji wake ni Pierluigi Collina, ambaye sasa Mkuu wa Marefa wa UEFA, na Gianni Infantino, Katibu Mkuu wa UEFA.
Kikao hiki hujadili Msimu mpya wa Mashindano ya Klabu ya UEFA na makocha hupewa mafunzo kuhusu Mashindano hayo hasusan Sheria au Kanuni mpya.
0 comments:
Post a Comment