Uingereza yaanza vizuri kufuzu EURO 2016,pata matokeo mengine.
Michezo ya kufuzu EURO 2016 imeendelea tena jana na Katika Mechi ya kwanza ya Kundi E iliyochezwa St Jakob Park Mjini Basel, Wenyeji Uswisi walifungwa mabao 2-0 na UingerezaUingereza walipata Bao lao la kwanza katika Dakika ya 58 kupitia Danny Welbeck baada ya nahodha Wayne Rooney kuunasa Mpira upande wake wa Uwanja na kupanda juu kisha kumpa pande safi Raheem Sterling alyempasia Welbeck na kufunga kwa ugoko.
Bao la Pili la Uingereza lilifungwa Dakika ya 94 tena na Danny Welbeck baada Rickie Lambert, alieingizwa kuchukua nafasi ya Rooney, kumpasia Sterling ambaye alimsogezea Welbeck na kumalizia.
MATOKEO:
Jumatatu Septemba 8
Russia 4 Liechtenstein 0
Luxembourg 1 Belarus 1
Austria 1 Sweden 1
San Marino 0 Lithuania 2
Spain 5 Macedonia 1
Estonia 1 Slovenia 0
Switzerland 0 England 2
Ukraine 0 Slovakia 1
Montenegro 2 Moldova 0
Mechi za Makundi EURO 2016 zinaendelea Jumanne Usiku.
Jumanne Septemba 9
Kazakhstan v Latvia
Azerbaijan v Bulgaria
Croatia v Malta
Norway v Italy
Czech Republic v Netherlands
Iceland v Turkey
Andorra v Wales
Israel v Belgium
0 comments:
Post a Comment