Tuesday, 30 September 2014

Valdes atafanyiwa vipimo vya afya wiki ijayo ili kujiunga na Liverpool.

Klabu ya Liverpool  iko mbioni kumsajili golkipa  mhispania  Victor Valdes, baada ya kupona jeraha la goti.

Taarifa zilizonaswa na Sports4lifeTz ni kwamba Kipa huyo wa zamani wa Barcelona mkataba wake ulimalizika ndani ya klabu hiyo na uhamisho wa kwenda Monaco uliingia dosari baada ya kupata jeraha hilo.

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amedai kuwa kipa Simon Mignolet  hafanyi vizuri kwa sasa na usajili wa Valdes unamaanisha kuwa Mignolet atapata changamoto.

Valdes mwenye miaka  32 atafanyiwa vipimo vya afya wiki ijayo ili kuangalia kama amepona vizuri.

0 comments:

Post a Comment