Manchester United na Chelsea kupambana ili kumnasa Coleman,Fellaini itakula kwake.
Klabu ya Manchester United iko kwenye mpango wa kumnunua mlinzi wa Everton Seamus Coleman wakati huo Marouane Fellaini atahusishwa katika mpango huo.
Van Gaal atapambana na Mourinho katika dili hilo.
Imeelezwa kuwa Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ameridhishwa na kiwango na mchezaji huyo mwenye miaka 25 na atasajiliwa katika usajili wa mwezi Januari.
Manchester United imesema kuwa itamrudisha kiungo wake ambaye ameshuka kiwango Marouane Fellaini katika viunga vya Goodison Park.
Fellaini alijiunga na Manchester United akitokea Everton msimu wa mwaka 2013, wakati huo Red Devils wakifundishwa na David Moyes, lakini (Fellaini) alishindwa kung'aa ndani ya Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment