Van Gaal aendelea kununua wachezaji wa Argentina,ameandaa £40 kwa ajili ya Otamendi.
Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal bado anaendelea na harakati za kutengeneza nafasi ya ulinzi baada ya klabu yake kuteseka kulinda mabao baada ya kichapo cha 4-0 na 5-3dhidi ya MK Dons na Leicester City.Katika kuepuka aibu hiyo Van Gaal anajiandaa kumnunua Nicolas Otamendi.
Mlinzi huyo raia wa Argentina ameaandaliwa kiasi cha £40 million na Van Gaal.
Mashabiki wa United wanashangaa iweje mholanzi huyo amnunue beki huyo kwa £40 wakati Valencia ilitoa kiasi cha £9.5 million kwa mlinzi huyo mwezi February kutoka Porto.
Lakini ripoti huko Hispania zinadai kuwa Valencia haitamuuza Otamendi, ingawa United iko tayari kutoa £40 million.
Otamendi akifanikiwa kutua Old Traford ataungana na Rojo pamoja na Di Maria wakiwa ni raia wa Argentina.
0 comments:
Post a Comment