Saturday, 20 September 2014

VPL kuanza leo timu 12 viwanja 6 alama 3 muhimu.....

Mshikemshike wa Ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 unaanza  leo kwa mechi sita timu 12 kuwania alama tatu muhimu  nchini.

Katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro  Mtibwa Sugar watakuwa nyumbani kuwakaribisha Washindi wa Ngao ya Jamii msimu wa 2014/2015  Yanga ya Dar es salaam.

Kuelekea mpambano huo Mtibwa kupitia msemaji wake Tobias Kifaru imesema lazima iwafunge Yanga na hawataogopa vitisho vya mashabiki wa Yanga kuhusu Jaja.

Hiyo inakuja baada ya  majina ya Wabrazil wawili, Genilson Santos Santana ‘Jaja’ na Andrey Coutinho kuwa gumzo huku jezi zao zikiongoza kuuzwa.

Mechi nyingine leo hii ni baina ya mabingwa watetezi, Azam fc ambao watakuwa uwanja wa nyumbani wa Azam Complex kuchuana na Polisi Morogoro.

Stand United itakuwa uwanja wa nyumbani wa Kambarage mjini Shinyinga kuoneshana kazi na wageni wenzao, Ndanda fc kutoka mkoani Mtwara.

Katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga, wenyeji Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera.

Maafande wa Ruvu Shootings watasaka pointi tatu muhimu mbele ya Tanzania Prisons  katika uwanja wa Mabatini, Mlandizi, mkoani Pwani.

Mechi nyingine kali itapigwa uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ambapo wenyeji Mbeya City wanaikaribisha JKT Ruvu ya Pwani.

Ligi hiyo itaendelea kwa mechi moja kupigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa kuwakutanisha Simba sc dhidi ya Coastal Union.

0 comments:

Post a Comment