AC Milan yasema kuwa Essien hana Ebola.
Klabu ya AC Milan ya nchini Italia imekanusha taarifa zinazodai kuwa nyota wa Ghana Michael Essien amepata ugonjwa wa Ebola akiwa katika majukumu ya timu ya taifa.Ripoti mbalimbali nchini Ghana kuanzia jana zinadai kuwa Essien amepata virusi vya Ebola.
Klabu hiyo ya Serie A imetoa taarifa kuwa inakanusha taarifa hizo kuhusiana na mchezaji wao.
Gazeti la The Daily Times na Newswire NGR zote kutoka Nigeria zilitoa taarifa hizo ambazo zimekanushwa waziwazi na AC Milan.
Wakati hayo yakiendelea uongozi umedai kuwa hakuna kiongozi aliyezungumzia hilo huku mchezaji mwenyewe akisema kuwa hana tatizo lolote.
"Ebola ni ugonjwa hatari mno watu wasifanye masihara kabisa na ugonjwa huo,aliyeandika taarifa hizo hana weledi wowote na kazi yake!!!" alisema Essien.
Mashabiki wa Essien wameomba hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya vyombo hivyo vya habari.
0 comments:
Post a Comment