Hakuna wa kufananishwa na Ronaldo kwa sasa-Kroos.
Nyota wa klabu ya Real Madrid Toni Kroos anaamini kuwa hakuna mchezaji bora wa dunia kwa sasa zaidi ya Cristiano Ronaldo na kusema kuwa yeye ndo kilichomfanya ajiunge na Real Madrid.Kroos ameshuhudia Ronaldo akifunga mabao 17 katika michezo 11 msimu huu baada ya kujinga na mabingwa hao wa Ulaya akitokea Bayern Munich.
Ingawa kuna vipaji vingi Madrid, Kroos amesisitiza kuwa wao ni kama familia kule Santiago Bernabeu na kusema kuwa Ronaldo ni nguzo muhimu katika familia hiyo.
"Nina furahi kucheza ndani ya Madrid. Ingawa watu hawana imani juu yangu,ila watu wa Madrid wana imani na mimi." alisema Kroos.
Kroos amekiri kuwa kwa sasa anaongea vizuri lugha ya kiingereza na kocha Carlo Ancelotti.
Amedai kuwa si rahisi kuwaelewa wachezaji wote kwa kile wanachokizungumza ila anaelewa vitu muhimu vinavyozungumzawa klabuni hapo.
0 comments:
Post a Comment