Monday, 6 October 2014

Falcao atamani kubaki Old Traford.

Mshambuliaji Radamel Falcao amekiri kuwa anataka abakie na Klabu hiyo moja kwa moja badala ya Msimu mmoja kama Mkopo wake toka AS Monaco unavyotaka.

Falcao alifunga Bao lake la kwanza kwa Man United na hilo lilikuwa Bao la Pili na la ushindi kwenye Mechi ambayo United iliifunga Everton 2-1 Uwanjani Old Trafford jana jumapili.

Falcao yuko kwa Mkopo wa Msimu mmoja lakini Mkataba wake unaruhusu Man United kumnunua moja kwa moja ikiwa watalipa Pauni Milioni 43.

Akiongea na Kituo cha TV cha Man United(MUTV) Falcao alisema: “Mimi na Familia yangu tuna furaha hapa na tunataka tubaki kwa Miaka mingi hapa!”

Ligi Kuu Uingereza itapumzika kwa muda kupisha Mechi za Kimataifa na itarejea  Wikiendi ya Oktoba 18 lakini Man United watacheza Oktoba 20 Ugenini na West Bromwich Albion.

0 comments:

Post a Comment