Mashindano ya Vijana U12 kufanyika Mwanza.
Mashindano ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 12 yatafanyika Desemba mwaka huu jijini Mwanza.
Akizungumza wakati wa kutangaza mpango wa programu ya vijana inayolenga Fainali za Afrika za U17 mwaka 2019 ambapo Tanzania imeomba kuwa mwenyeji, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema mashindano hayo yatashirikisha kombaini za mikoa yote.
Mashindano
hayo yatafanyika kuanzia Desemba 6 hadi 12 Mmwaka huu, na timu
zinatakiwa kuwasili jijini Mwanza, Desemba 5 mwaka huu. Bajeti ya
mashindano hayo ni sh. milioni 350.
Rais
Malinzi aliwashukuru wakurugenzi wa shule za Alliance (James Bwire) na
Lord Baden Powell (Kanali mstaafu Idd Kipingu) kwa kukubali shule zao
kuwa za kwanza kuanzia programu hiyo ya vijana.
Pia
aliishukuru kampuni ya Symbion ambayo imetoa sh. milioni 100 kwa ajili
ya kuunga mkono mashindano hayo ya U12. Symbion ni moja ya wadau
wanaoshirikiana na TFF katika mpango wa miaka mitano ya programu za
vijana.
Mkurugenzi wa Symbion, Stewart John Hall aliwasilisha kwa waandishi wa habari programu hiyo ambayo imeambatanishw.
0 comments:
Post a Comment