Thursday, 2 October 2014

Ferguson hana lawama hata kidogo-Rio Ferdinand.

Rio Ferdinand


Beki maarufu wa zamani wa miamba wa Uingereza Manchester United, amemfagilia  mwalimu mstaafu Sir Alex Ferguson kutokana na aibu inayokumba na vigogo hao wakati huu. 
 
United waliporomoka sana  baada ya kuwika katika mchezo wa ngazi ya juu Uingereza kwa zaidi ya miongo miwili walipomaliza nafasi ya  saba msimu wa mwaka jana chini ya  ya utawala wa David Moyes, ambaye alimrithi  Ferguson.

Kocha mpya, Louis Van Gaal, ameshindwa kurudisha hadhi ya klabu hiyo na kuzua hisia kuwa Ferguson aliacha klabu hicho katika hali mbaya zaidi baada ya kukiongoza kushinda taji la Uingereza  la msimu wa 2012/13.

Kulingana na Ferdinand ambaye aliondoka United mwishoni mwa msimu uliopita  alikanusha vikali tetesi kwamba Moyes alirithi kikosi kibovu kutoka Ferguson.

“Sielewi sababu ya kusema hivyo kwani kulikuwa na wachezaji wakuu walioshinda ligi alama 11 mbele ya waliofuata. Ni lazima uwe timu bora kufikia utukufu huo.

“Basi mambo yalianza kuporomoka lini? Ni sababu ya Ferguson? Watu wanadaiaje hilo? Sifikirii lawama lielekezwe kwa  Ferguson na kuondoka kwake baada ya kushinda taji ni jambo bora sana,” Ferdinand ambaye anachezea QPR aliongeza.

0 comments:

Post a Comment