Thursday, 2 October 2014

Dani Alves kutimkia Manchester United au Liverpool msimu ujao.

Beki wa upande wa kulia wa klabu ya Barcelona  Dani Alves  amesema kuwa msimu ujao atajiunga na klabu ya ligi kuu ya Uingereza.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka  31 anahusishwa sana kujiunga na vilabu vya Uingereza na mapema mwezi Juni alisaini mkataba wa mwaka moja tu na Barcelona.

Raia huyo wa Brazil ameshinda mataji 16 akiwa  Barcelona baada ya kujiunga kutoka  Sevilla mwaka 2008,kwa sasa hajakubali kusaini mwaka mwingine akidai kuwa mwakani atahitaji zaidi kucheza Uingereza.

"Nitakwenda kucheza Uingereza msimu ujao" alisema Alves kupitia gazeti la O Globo."Ninakwenda kucheza sehemu ambapo soka lipo.Huu utakuwa mwaka wangu wa mwisho ndani ya Barca."

Alves hajaweka wazi ni klabu gani ataenda kuitumikia lakini Liverpool na  Manchester United wamehusishwa sana katika kumsajili Alves.

Alves amecheza michezo 303  ndani ya Barcelona na kufunga mabao  20 na kutoa pasi  85 zilizozaa mabao.

0 comments:

Post a Comment