Thursday, 9 October 2014

Sir Alex Ferguson asema Van Gaal anafaa sana Manchester United.

Akiongea kwa mara ya kwanza tokea Louis van Gaal awe kocha wa klabu ya Manchester United,kocha aliyestaafu Sir Alex Ferguson ameunga mkono uamuzi wa kocha huyo kukarabati Kikosi cha Manchester United na pia kudai kuwa kocha huyo mpya ameanza vyema sana himaya yake.

Ferguson amesema kuwa amevutiwa mno na jinsi Mholanzi huyo anavyoiongoza Timu na kuongeza kuwa Van Gaal ana kila haki kuunda Kikosi chake mwenyewe kitakachobeba falsafa yake.

Tangu atue, Van Gaal amekifumua kile Kikosi ambacho kilitwaa Ubingwa wa Uingereza kwa mara ya mwisho chini ya Msimu wa mwisho wa Sir Alex Ferguson, 2012/13 huku Wachezaji 14 wakiondoka Klabuni hapo, miongoni mwao wakiwemo Danny Welbeck, Nemanja Vidic, Rio Ferdinand na Patrice Evra, na kutumia kitita cha Pauni Milioni 150 kuwanunua Wachezaji wapya 6.

Akiongea kwenye Kipindi maalum na Kituo cha TV cha Man United (MUTV,), Ferguson amesema kuwa Louis van Gaal amefanya mabadiliko makubwa huku kuisafisha Timu na kujenga Timu yake mwenyewe.
Lakini Van Gaal alianza kwa kusuasua hasa kutokana na nafasi ya ulinzi kuwa mbovu kiasi cha kupoteza uongozi wa mabao 3 na kupigwa mabao 5-3 na Leicester City Mwezi uliopita.

Lakini tangu wakati huo Kikosi cha Van Gaal kimebadilika polepole licha ya kuwa na Majeruhi wengi na kuweza kupanda hadi Nafasi ya 4 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Uingereza.

0 comments:

Post a Comment