Madereva wa Langalanga waja juu kuhusu ajali ya Bianchi.
Mwendesha magari wa mashindano ya langalanga kutoka timu ya Force India, Sergio Perez amedai kuwa ajali iliyomuacha dereva Jules Bianchi na majeraha ya kichwa, haikubali na iliweza kuepukika.Perez ambaye ni raia wa Mexico amesema madereva lazima watalitaka shirikisho la mashindano hayo-FIA kutaka ufafanuzi wa kile kilichotokea na hatua zitachukuliwa kuepuka hali hiyo.
Perez aliendelea kudai kuwa wanapaswa kupewa majibu ya kina wa kitu gani haswa kilitokea katika ajali hiyo mbaya.
Bianchi kwasasa anaendelea vyema ingawa bado yuko katika chumba cha uangalizi maalumu baada ya gari lake kupoteza mwelekeo na kuligonga trekta lililokuwa pembezoni wakati mashindano ya Japan Grand Prix Jumapili iliyopita. Perez amesema inatakiwa hatua mpya za makusudi zichukuliwe ili kuwepo na gari la usalama popote ambapo trekta linatumika kwa ajili ya kuondoa magari yaliyopata hitilafu lkatika mashindano hayo ili kuepuka kujirudia kwa ajali kama hiyo.
0 comments:
Post a Comment